Uchanganuzi wa Majina ya Wanaume katika Jamii ya Watugen

Not scheduled
15m
Abstract for Research Paper Lugha na Maendeleo katika Karne ya Ishirini na Moja

Description

Utafiti huu ulilenga kuchambua majina ya wanaume miongoni mwa wanajamii wa jamii ya Watugen kutoka eneo la Kaunti ya Baringo nchini Kenya, Afrika Mashariki. Japokuwa majina ya kipekee hujumuisha majina ya Mito, milima, vijiji, miji, wat una nchi, utafiti huu ulishughulikia majina ya wanaume pekee. Makala hii ina vijisehemu zifuatazo: Maelezo mafupi kuhusu jamii ya Watugen, utamaduni wa kupeana majina, sherehe za kupeana majina, Uusanyaji data, majina ya wanaume na maana zao na hitimisho. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya simiotiki. Nadharia ya simiotiki hushikilia kwamba kila ishara ina maana yake maalum. Ukusanyaji wa data ulifanyika nyanjani. Mbinu ya mahojiano ilitumika kukusanya data na sampuli ya majina yaliorodheshwa kwenye majedwali. Maswali yafuatayo yaliongoza utafiti huu; Watugen ni watu wapi? Sherehe zipi ziliambana na kupeana majina? Sababu za ujinaishaji, kategoria zipi zilikuwepo?miundo ya majina hayo yalikuwaje? Maana za majina ya wanaume yalikuwa na maana zipi? Majibu ya maswali haya ni kiini cha utafiti huu.Maotokeo ya utafiti yalidhihirisha kwamba majina ya wanaume yalitokana na hali halisi katika jamii ya Watugen na kila jina lilibeba maana maalum pia, ilibainika kwamba maajilio ya wageni aghalabu, wamisionari yaliathiri ujinaishaji kaika jamii ya Watugen. Aidha, ilibainika kwamba majina hayo miundo mbalimbali
Maneno muhumu: Majina ya wanaume, Maana ya majina, Sherehe za kupeana majina, Jamii na Simiotiki.

Primary author

Dr DAVE BOWEN (KABARAK UNIVERSITY)

Presentation Materials

There are no materials yet.

Peer reviewing

Paper