Kuwezeshwa kwa Uchumi kupitia Kiswahili

Not scheduled
20m
Abstract for Research Paper Lugha na Maendeleo katika Karne ya Ishirini na Moja

Description

Lugha ni nyenzo kuu ya mawasiliano katika jamii. Jamii ya Afrika mashariki kama jamii nyingine duniani zinajivunia lugha ya Kiswahili kama nyenzo mojawapo ya mawasiliano katika mataifa mengi ya Afrika mashariki. Lugha nyingine zinazozungumzwa Afrika masharika kando na lugha-mame za wazaliwa wa Afrika mashariki ni, Kiingereza, Kifaransa na Kijerumani. Lugha hizi zilizokuja na mkoloni pia zimepata nafasi kubwa katika jamii ya Afrika kwa ujumla. Siku za hivi karibuni kumeshuhudiwa ongezeko la matumizi ya lugha ya Kichina na mafunzo kutolewa kwa waafrika kwa lugha hii. Hata hivyo, lugha hizi zinaendelezwa kwa mtazamo na imani za waafrika wenyewe. Waafrika wengi wanaamini kuwa, maendeleo na kungeuka kunatokana na lugha hizi za kikoloni. Mitazamo hii ni tata na imelifanya bara la Afrika kuyumba kimaendeleo. Maendeleo huanza kupitia kwa mawasiliano ambapo mawasiliano hayo hudhibitiwa na lugha ya wazungumzaji. Kupitia lugha hizi za kigeni basi, kuna mkachanganyiko na hivyo kulemaza mawasiliano katika jamii ya Afrika. Lugha kama zao la kijamii huleta umoja miongoni mwa wanajamii kutokana na kule kuelewana katika matumizi ya istilahi pamoja na utamaduni sawa. Kuwepo kwa lugha nyingi za kigeni na ambazo zinashabikiwa sana na waafrika, kumedumaza mawasiliano na hivyo kurejesha nyuma maendeleo. Baadhi ya nchi za Afrika zinatumia lugha za kikoloni kama lugha zao rasmi. Hili linalazimisha yeyote anayezuru nchi hizi ajifunze lugha yao ili kuwepo mawasiliano. Hivyo, makala haya yanalenga kuangazia juhudi za nchi za Afrika mashariki na bara la Afrika kutumia Kiswahili kama nyenzo ya mawasiliono miongoni mwao ili kurahisisha mawasiliano na biashara kati ya w

Istilahi muhimu,Lugha, Utamaduni, Mawasiliano.Maendeleo

Primary author

Dr angela sawe (lecturer)

Presentation Materials

There are no materials yet.