VIGEZO VYA HYMES VYA MAWASILIANO: UCHANGANUZI WA MATUKIO KWENYE HAFLA YA MAHARI KATIKA JAMII YA GIKUYU

Not scheduled
20m
Abstract for Research Paper Dynamics in English and other Foreign Languages

Description

VIGEZO VYA HYMES VYA MAWASILIANO: UCHANGANUZI WA MATUKIO KWENYE HAFLA YA MAHARI KATIKA JAMII YA GIKUYU
Kariithi Francis
Department of Languages, Linguistics and Literature
Kisii University, Kenya

Ikisiri
Lugha ni asasi muhimu katika mfumo mzima wa mawasiliano ya mwanadamu ulimwenguni ambapo ndanimwe mna viambajengo vinavyoukamilisha usarufi wa lugha husika ambao kimsingi hufungamanishwa na usimbuzi wa yale yanayowasilishwa na mwanajamii lugha yeyote yule. Ikumbukwe kuwa lugha na jamii ni shilingi kwa ya pili; bila lugha hamna jamii na bila jamii hamna lugha yoyote ambayo itarejelewa. Lugha kama asasi inajitokeza bayana kama kiunzi muhimu kinacholipambanua kundi fulani la watu kiutamaduni, kijamii na hata kitaifa. Kwa mujibu wa mantiki hii, lugha hukuzwa na kuendelezwa na jamii na ni kutokana na mwelekeo huu ambapo jamii hutazamwa kama kundi la watu wenye mwingiliano mpevu wa imani fulani, utamaduni, malengo, mitazamo na vionjo vyake. Lugha huchukua nafasi muhimu katika kuusokotoa utata ambao hughubika sherehe hiyo muhimu ambayo huongozwa na utaratibu Wa jamii lengwa. Sherehe za posa katika jamii ya Agikuyu zinaenziwa sana tangu enzi za mababu zetu ambapo pande zote mbili; ule wa anayechumbiana na ule wa anayechumbiwa waliwahusisha wazee waliokuwa wamebobea na kutopea katika shughuli hiyo. Hata sasa wazee wanaoyawakilisha makundi haya huwa wanasheheni tajriba ya kina; umilisi wa lugha ya jamii husika ukiwa kigezo muhimu – yaani mlumbi. Utafiti ulibainisha kuwa, matukio asili ya usemi yalichochewa na hali husika yakifungamanishwa na muktadha kwa mujibu wa lugha ya jamii hiyo. Utafiti ulibainisha pia kuwa matukio yaliyojikariri sana yalikuwa ya kuujenga usuhuba (umoja), kuomba ushauri, kujenga imani, matumizi ya chuku miongoni mwa hali zingine. Kwa mujibu wa vigezo vyake Hyme’s (1974) vya ethnografia ya Mawasiliano, MWALEKIHAMKANYA (SPEAKING) kunayo matukio kadhaa yanayoathiri kila hali ya usemi kwenye mchakato mzima wa hafla hii muhimu katika jamii ya Agikuyu.
Maneno Msingi:
MWALEKI HAMKANYA, Ethnografia ya Mawasiliano, Jamii Lugha, Utamaduni

Primary author

Francis Kariithi (Lecturer, Kisii University)

Presentation Materials

There are no materials yet.