Sitiari Dhanifu Katika Mazungumzo ya Hafla ya Mahari Katika Jamii ya Agikuyu

Not scheduled
20m
Abstract for Research Paper Dynamics in English and other Foreign Languages

Description

Ikisiri
Utafiti huu unajikita katika kuzitathmini isitiari dhanifu ambazo huibuka katika mchakato mzima ambao hufungamanishwa na hafla za majadiliano ya mahari katika awamu mbalimbali za shughuli hiyo muhimu katika jamii ya Agikuyu inayorejelewa kama “Ruracio”. Matumizi ya sitiari katika kujenga majadiliano huwa uti wa mgongo na kwa sababu hiyo wawakilishi wanaoteuliwa na pande mbili za aila husika huhitajiwa kuwa na umilisi mpevu wa lugha hii ili kufaulisha shughuli hiyo. Ikumbukwe kuwa sitiari zinazotumiwa katika mchakato husika huchangia kujenga ukuruba baina ya koo husika kwa mujibu wa mila na desturi za jamii ya Agikuyu popote pale inapojikuta. Data iliyokusanywa ilirekodiwa kutoka mazungumzo halisi ya hafla husika ambapo mtafiti alivihudhuria vikao vitano tofauti lengo likiwa kuipata data ambayo kwa mujibu wa utafiti ingesemwa kuwa tegemevu. Kama mshiriki, mtafiti alizihudhuria hafla mbili katika gatuzi la Muranga na tatu kati ya hizo katika gatuzi la Nakuru anakokaa. Data ilitafsiriwa na kuanishwa kwa mujibu wa mara tokezi na hatimaye kuelezewa. Sitiari nyingi ziliendana na kujenga vitambulisho vya kijinsia ambapo mseto wa sitiari ulibainika kulenga matukio tofautitofauti ya mchakato wote wa sherehe hii. Ilibainika kuwa sitiari husheheni hafla hii zikichangia kuingiliana na kukamilisha awamu tofautitofauti katika mitagusano ya jamii hii ya Agikuyu. Matokeo ya utafiti huu bila shaka yatajenga dafina bora ya wasomi katika uwanja wa uchanganuzi lugha. Baadhi ya sitiari zilizojitokeza katika hafla husika zilikuwa sitiari fiche, sitiari fifi, sitiari changamano, sitiari mseto, sitari kuu, sitiari shehenezi, sitiari thabiti, sitiari za hisimseto na sitiari kitashihisi ambazo ziliingiliana na mila na desturi za jamiilugha hii.
Maneno Msingi: Sitiari Dhanifu, jamiilugha, Utamaduni,.

Primary author

Francis Kariithi (Lecturer, Kisii University)

Presentation Materials

There are no materials yet.